IRAMBA - SINGIDA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Martha Mlata amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Kata ya Kidaru wilayani Iramba mkoani Singida kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambae amejitoa kwa dhati kuwaletea maendeleo na kuwainua kiuchumi.
Mlata ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliyofanyika katika kata hiyo wilayani hapa.
"Dk. Samia hapajui Kidaru lakini fedha zilizojenga kituo cha afya na chenye vifaa vya kisasa takribani Sh milioni 500, umeme na maji yakiwemo madarasa yakisasa amewaletea kupitia wawakilishi wake, hivyo tuendelee kumuamini Rais wetu, " amesisitiza na kuongeza kuwa:
"Endeleeni kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa sababu kikiahidi kinatekeleza na Rais Dk. Samia atakapokuja Singida akiwa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa chama hichi nitamlete hapa kidaru aione furaha yenu, shukrani, ahadi na pongezi zenu."