DC Mpogolo wenye viashiria vya uvunjifu wa amani waripotiwe



MKUU  wa Wilaya  ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka viongozi wa dini,  vyama vya siasa na serikali kushirikiana kuhakikisha amani, utulivu, upendo na umoja vinalindwa.

Aidha, ametaka mtu yoyote akiona viashiria vya uvunjifu wa amani atoe taarifa kabla ya vitendo hivyo havijaleta madhara katika jamii na wahusika wachukuliwe hatua.

Mpogolo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza  na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kata tisa za Jimbo la  Ilala akiwa katika ziara yake ya kusikililiza, kutatu kero na kuhamasisha ushiriki wa katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mpogolo ameeleza tunu ya amani, umoja na mshikamano imeendelea kulindwa na Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema viongozi wa ngazi zote wawe sehemu ya kuilinda tunu hiyo na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa yeyote anayetaka kuhatarisha amani ili achukuliwe hatua mapema. 

Amehimiza viongozi wa Chama na serikali kuhakikisha kila mtanzania mwenye sifa ya kujiandikisha na kupiga kura anajiandisha katika daftari la mkazi serikali za mitaa litaloanza mwezi ujao tarehe 11 hadi 20.