MWENYEKITI RAJAB AMSHUKURU RAIS SAMIA KUIFUNGUA TANGA KIUCHUMI

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amesema serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi hususan wanyonge, ndiyo maana imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwemo Mkoa wa Tanga kwa kujenga Bandari na viwanda.

Pia, amewataka wananchi  wa Mkoa wa Tanga kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa anazozifanya katika Mkoa huo, ambazo zimefungua ajira kwa vijana na kukuza uchumi.

Mwenyekiti Abdallah ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameyasema hayo Mkoani humo, jana, wakati akianza ziara yake ya situ tatu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda, alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kuboresha miradi ya uwekezaji ikiwemo Bandari ya Tanga kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM, Tanga, Suleiman Sangwa alimpongeza Mwenyekiti kwa ziara hiyo na wananchi kwa kuitikia kwa wingi katika ziara hiyo.