MWENYEKITI WA CCM TANGA AFUNGUA MASHINA YA VIJANA AWACHANGIA SH. MILIONI 15

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah ameanza ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa Tanga, huku akifungua mashina mawili ikiwemo Mgandini na aliwachangia sh.milioni 14 kushirikiana na viongozi wa Chama na serikali.

Akifungua matawi hayo katika jimbo la Tanga Mjini, amewasisitiza vijana kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuendeleza miradi ya kiuchumi inayotoa ajira kwa vijana.

Pia, amewapongeza vijana kwa kuendelea kujishughulisha kiuchumi kutafuta kipato kwa njia halali huku akiahidi kuendelea kuwaunga Mkono.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk.Batilda Burian, amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo uwekezaji wa viwanda na Bandari, ambavyo vimeendelea kuchochea uzalishaji wa ajira na kukuza uchumi.