MKT WA CCM TANGA AKABIDHI SH.MILIONI 50 KUKARABATI UWANJA WA MKWAKWANI KUKIDHI VIGEZO VYA FIFA


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, amekabidhi sh.milioni 50 kukarabati ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Mkwakwani uliopo mkoani humo kukidhi vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) na kutumika kuchezewa michezo ya Kimataifa.

Mwenyekiti Rajab amekabidhi fedha hizo, kwa Katibu wa Chama Mkoa huo huku akiwataka wananchi na wadau wa michezo kuunga mkono jitihada hizo za kukuza michezo mkoani humo.

"Tumekabidhi fedha hizi sh.milioni 50, kwa lengo la kuboresha uwanja wetu wa Mkwakwani, tunaamini ukarabati huu ukikamilika uwanja huu utakuwa na vigezo vya FIFA, hivyo kutumika kuchezea michezo ya Kimataifa," alisema.

Vilevile, amesema kutoa fedha hizo ni kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kuendeleza michezo nchini na kusaidia vipqji Cha vijana.