Na MWANDISHI WETU
TAASISI ya Doris Mollel (DMF), imemkabidhi Mariam Mwakabungu (26), nyumba ya makazi Kwa moyo wake wa kujitolea kukumbatia Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Amana, yenye thamani ya sh. milioni 45 iliyopo Chanika – Zavara jijini Dar es Salaam.
Nyumba hiyo aliyozawadiwa na msamaria mwema (hajataka kutajwa jina) imejengwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine waliochangia baadhi ya vitu wakati wa ujenzi wake.
Alikabidhiwa nyumba hiyo Jumapili, Novemba 17, 2024 kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Mariam aliyefikishwa eneo hilo akiwa amefungwa kitambaa usoni akiwa na mume wake, Christopher Nyoni (30).
Ikumbukwe kuwa pamoja na nyumba hiyo, Julai 20, 2023 Serikali kupitia Wizara ya Afya, ilitoa ajira ya mkataba kwa Mariam, ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za pongezi zilizoambatana na fedha taslimu Sh2 milioni.