MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amekabidhi vyeti kwa madereva 600, wa vyombo vya usafirishaji waliohitimu mafunzo hayo baada ya kuwalipia sh.milioni 30 katika Chuo Cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) Tanga.
Akikabidhi vyeti hivyo, jijini Tanga, Mwenyekiti Abdallah, aliwapongeza madereva hap kwa kuhitimu mafunzo hayo yaliyowawezesha kupata vyeti hivyo na kuwa madereva mahiri.
"Nawapongeza kwa hatua hii muhimu na kubwa katika fani yenu, wote kwa pamoja kwa kukubali kupata mafunzo hayo ya miezi mitatu hadi kuhitimu na leo tunawakabidhi vyeti, hongereni sana, sasa tunaamini mtaenda kuwa madereva bora na himara kwani mmetimiza vigezo", amesema.
Pia, Mwenyekiti Abdallah amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kuwapa maagizo viongozi wa Chama, kuwakimbilia wananchi wanyonge wa hali ya chini huku akiahidi kuendelea kutekeleza hilo.