BALOZI MULAMULA AMLILIA MAFURU AKITAJA USHAURI WAKE KATIKA DIPLOMASIA YA UCHUMI

MBUNGE, Balozi Liberata Mulamula ameungana na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Lawrence Mafuru, huku akisema Taifa limepoteza mtu muhimu na tunu ya taifa, ambaye alikuwa na mchango mkubwa serikali na kwa mtu mmoja mmoja.

Tukio la kuaga mwili wa marehemu Mafuru lilifanyika Karimjee jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

Balozi Mulamula alisema "Nitamkumbuka marehemu Mafuru, kwani wakati wa uhai wake, tulikuwa tunakutana sana na kunipa ushauri kila wakati kuhusiana na Diplomasia ya uchumi na mpango wa Dira ya Taifa,".

Alisema Taifa litamkumbuka Mafuru kwa mchango wake kupitia utumishi wake uliotukuka, pia, jamii itamkumbuka kwa vile alivyogusa maisha ya mtu mmoja mmoja.