KIGAHE AENDELEA KUIFUNGUA MUFINDI KASKAZINI KWA UJENZI WA BARABARA



Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Mufindi Kaskazini, Exaud Kigahe, amesisitiza kuwa ataendelea kuifungua Mufindi Kaskazini kwa kukarabati barabara zote korofi jimboni humo kwa kiwango cha zege na lami, kurahisisha usafiri na kuchochea ukuaji uchumi.

Kigahe ameyasema hayo, hivi karibuni alipokuwa akikagua ukarabati wa ujenzi wa barabara zinazotekelezwa kwa kiwango cha zege na lami.

"Kazi inaendelea sehemu kubwa ya Jimbo la Mufindi Kaskazini kujengwa kwa kiwango cha zege hususan maeneo korofi, ikiwemo Barabara ya Kinyanambo C hadi Kisusa Jimbo la Mufindi Kaskazini," alisema.

Pia, aliishukuru Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu mbalimbali huku akiwataka wananchi kumuunga mkono na kujiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.