Na MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amevuna wanachama wote wa Chama Cha Wananchi (CUF), katika Kata ya Kwale Wilaya ya Mkinga, mkoani humo.
Hayo yamejili mkoani Tanga, wakati Mwenyekiti Rajab Abdallah akiendelea na ziara katika Wilaya ya Mkinga ikiwa ni sehemu ya kujiandaa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Tunaendelea na ziara mkoani hapa, Leo tupo hapa Wilaya ya Mkinga, tunaendelea kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kutatua changamoto za wananchi, wakati tunaelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu," amesema.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Rajab aliwasisitiza wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuwachagua wenyeviti wa serikali za mitaa utakao fanyika Novemba 27, na kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia kwa kumuombea afya njema.