MJUMBE WA KAMATI KUU CCM, RAJAB ABDALLAH KUUNGURUMA LEO ARUSHA



Mjumbe wa Kamati Kuu, Rajab Abdallah ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha, anatarajiwa kuunguruma leo, mkoani humo, kunadi wagombea wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumatano Novemba 27.

Ziara hiyo ya Arusha, inafanyika baada ya mfululizo wa ziara ya siku nne iliyofanywa na Mwenyekiti Abdallah Katika Mkoa wa Tanga kupitia Wilaya nne za Korogwe, Handeni, Kilindi.

"Baada ya siku tatu mfululizo kuwashamoto katika Wilaya nne za Tanga na sasa tunaenda kuwashamoto mkoani Arusha kwa siku tatu, kutafuta kura kwa wagombea, wetu," amesema.

Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo mbalimbali nchini, zilizinduliwa Novemba 20 zinatarajia kuhitimishwa Jumanne Novemba 26 ambapo Uchaguzi ni jumatano Novemba 27.