MASHINDANO YA BULYANHULU HEALTHY LIFESTYLE MARATHON YAVUTA WENGI

Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare, akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon zilizoandaliwa na mgodi huo na kufanyika jana.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon baada ya kumalizika mashindano hayo mwishoni mwa wiki yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Baadhi ya washiriki wa mbio za Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon baada ya kumalizika mashindano hayo mwishoni mwa wiki yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu.


Meneja Mkuu wa Mgodi wa  wa Bulyanhulu, Cheick Sangare(aliyevaa kofia), akikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mshindi wa mbio za kilomita 42 ndefu Elias Charles.Mashindano ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon yalifanyika jana katika maeneo ya mgodi huo na kujumuisha wafanyakazi wa Mgodi,Wakandarasi na wakazi wa vijiji jirani.

                                                                ********************

Mashindano ya mbio ya kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon yaliyoandaliwa na  Mgodi wa dhahabu wa  Barrick Bulyanhulu yamefanyika jana ambapo Elias Charles, ameibuka mshindi wa jumla wa mbio ndefu  na kujishindia zawadi  ya baiskeli ya kisasa ya kupanda  milima aina ya La Ruta 29+.

Mashindano hayo ya mbio zenye urefu wa aina mbalimbali yamewashirikisha washiriki  zaidi ya 250 ambao ni wafanyakazi wa Mgodi, wakandarasi  wa Mgodi na wananchi wanaoishi kwenye  vitongoji vinavyozunguka Mgodi.

Zawadi nyingine ambazo wamejinyakulia  washindi katika mbio za Kilometa 21, 15, 10 na 5, ni pamoja na: friji; simu janja; saa ya kisasa,  mikeka ya mazoezi ya yoga na mashine za kutengeneza salasi na kukamua juisi. 

Mgeni rasmi katika hafla alikuwa  ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya, ambaye pamoja na kuwapongeza washiriki hao alisema kuwa ofisi yake itashirikiana na Mgodi katika kuhakikisha watumishi na wakandarasi wake wanapata miongozo ya lishe ya taifa ambayo kwa sasa imeanza kutumika katika ngazi zote kuanzia Serikali kuu hadi kwenye kata na vijiji.”Unene na kasi ya magonjwa yatokanayo na mifumo ya maisha yanaongezaka hivyo Serikali imeamua kulivalia njuga changamoto hii.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa  wa Bulyanhulu, Cheick Sangare,alisema kuwa kampuni imejipanga kuhakikisha kuwa suala la afya za wafanyakazi inalipa kipaumbele kwa kuwa inaamini kuwa kuwa na nguvu kazi yenye afya bora kunaleta tija zaidi.

Naye mtaalamu wa afya kutoka Mgodi huo, Dk. Nolask Kigodi, alisema mgodi ulikuwa na lengo la kupunguza uzito wa jumla wa kilo 1,500  kwa wafanyakazi wapatao 2,500 ikiwemo wakandarasi mbalimbali waliopo mgodini hapo. “Tumejipanga kuhakikisha suala la mazoezi linapewa kipaumbele sambamba na kuwa na sehemu za kufanyia mazoezi zenye vifaa mbalimbali na kuzingatia lishe bora.