WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, PROFESA MKENDA MGENI RASMI MAONYESHO TA KITAIFA YST 2022

Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST), Dk. Gozibert Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu Maonyesho ya Kitaifa ya taasisi hiyo yatakayofanyika, Desemba 8, mwaka huu, Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji wa Shirika la Karimjee Jivanjee Foundation, Caren Rowland, akizungumza kuhusu taasisi hiyo kuidhamini YST, kuelekea maonyesho hayo. 

 

                                                              ***************************

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonyesho ya Kitaifa ya Taasisi ya Young Scientists (YST) 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwanzilishi Mwenza wa taasisi hiyo, Dk. Gozibert Kamugisha, amesema maonyesho hayo yatafanyika Desemba 8, mwaka huuambayo yamepangwa kufanyika Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema YST imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha utafiti wa kisayansi na ugunduzi kwa vijana wa Shule za Sekondari kwa kipindi cha miaka 12.

Dk. Kamugisha amesema taasisi hiyo ni jukwaa la vijana kuonyesha ujuzi wao kisayansi  na imetoa fursa kwa wanafunzi kuvumbua njia za kisayansi kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.

Amesema mwaka huu idadi ya wanafunzi waliowasilisha maombi ya kufanya kazi za ugunduzi imeongezeka kwa kiasi kikubwa kufikia 1,143.

"Kati ya maombi 1,143 jumla ya kazi za utafiti na kisayansi 530 zimepitiwa usaidizi ambapo wanafunzi walioziandaa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuziboresha na hatimaye kazi kisayansi na ugunduzi 380 zimekamilika", amesema.

Kamugisha amesema kazi za kisayansi na teknolojia zitakazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni kuhusu njia salama ya kutunza mazao ya kilimo, kutunza mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji, dawa za asili na kuboresha afya za binadamu.

Pia maonyesho hayo yatajikita katika upatikanaji wa na uszalishaji wa nishati ya umeme, matumizi ya miziki katika kufundisha somo la hesabu mashuleni, matumizi ya mimea ya asili, kuboresha uzalishaji wa maziwa ya ng'ombe na kutatua tatizo la udumavu wa ukuaji wa kuku.

Naye Ofisa Mtendaji wa Shirika la Karimjee Jivanjee Foundation, Caren Rowland, amesema shirika hilo limekuwa mfadhili wa kujivunia kwa kuidhamini Young Scientist Tanzania (YST), kwa miaka 12 mfululizo.

Amesema Karimjee imeshadhamini wanafunzi 37 kufikia mwaka 2021 na itaendelea kudhamini, pia wanafunzi wanne watakaoshinda mwaka huu itafika idadi ya wanafunzi 41.

"YST wamefanya tukio la kipekee kwa ktoa jukwaa kwa vijana kutoka mikoa mbalimbali, kuonyesha ubunifu, ugunduzi na utafiti pamoja na talanta  zao za kisayansi, pia tunawapongeza YST kwa kuendeleza mpango huu wa kuchukua jukumu muhimu katika ukuzaji wa sayansi  Tanzania kwa kuhamasisha na kulea akili za vijana kote nchini", amesema.