WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM WAKIKAGUA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) WAKATI WAKIENDA DODOMA

Waziri  wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akizingumza na Wenyeviti wa CCM Mkoa, katika kituo cha treni cha Reli ya Kisasa (SGR), mkoani Morogoro, wakati wakikagua mradi huo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Kutoka kushoto ni Adam Kimbisa (Dodoma), Abbasi Mtemvu (Dar es Salaam) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma. (Picha na Muhidin Sufiani)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa (katikati), akifurahia jambo na Menyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaa, Abbas Mtemu, wakati waliposimama katika Kituo cha Treni ya SGR mjini Morogoro, walipokuwa katika ziara ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM wakishuka katika treni ya Mkandarasi Kituo cha Morogoro, wakati wakikagua mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia Treni ya Mkandarasi.