Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Camillus |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kunoresha na kuongeza ufanisi wa utendaji katika mikoa mitatu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime, imeeleza katika mabadiliko hayo, Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Fortunatus Muslim, kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Nafasi ya Fortunatus Muslim, inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Alex Mukama, ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkao wa Songwe.
Pia IGP Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Shadrack Masija, ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamnda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.