Faisal Salumu 'Fei Toto' |
NA MWANDISHI WETU
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza kuwa kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ bado ni mchezaji wa Yanga, kwa mujibu wa mkataba.
Kwa mujibu Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, uamuzi kamili wa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa kesho.
Alisema klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji wao, Feisal kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo pande zote (Yanga na Fei Toto) ziliwakilishwa na wanasheria wao.
Juzi, Fei Toto, alitinga TFF kusikiliza hilo akiwa na meneja wake ambaye ni baba yake mzazi pamoja na mwanasheria wake.