RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI NAMIBIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia, baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiagana na watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia, baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Namibia (Diaspora), katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na nchi zinazochangia vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB), uliofanyika nchini Namibia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi Namibia, baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Jijini Windhoek, nchini Namibia Mei, 8, 2023, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek, Namibia.