IGUNGA - TABORA
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Lucas Bugota amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali wilaya hiyo kwa kuipa miradi mingi ya maendeleo.
Bugota ametoa pongezi hizo wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kupokea taarifa ya hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 30, 2024, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
"Kwa dhati tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki kwa sababu tumepata miradi kila kona, hakika ameendelea kutujali," ameshukuru.
Aidha, Bugota amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selwa Abdalla Hamid kwa usimamizi madhubuti ambao umesaidia kuandaa na kukamilisha Rasimu ya Taarifa za mwisho za Hesabu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambazo zimeandaliwa kwa kuzingatia kanuni ya
31(4), LAAM 2019 ikiwemo matakwa ya mfumo mpya wa viwango vya kimataifa vya Hesabu za Sekta ya Umma.