KWA UWEKEZAJI HUU BANDARI YA DAR ES SALAAM ITAKUWA YA MFANO NA YA KUIGWA - MAKALLA

Na MWANDISHI WETU

"Niseme ukweli  Bandari ya Dar es salam ina mabadiliko makubwa sana kwani wakati nikiwa RC nilikuwa nakuja hapa lakini leo nimeshangaa ni utofauti mkubwa na  Chama cha Mapinduzi kinaipongeza Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zake kwa Uwekezaji mkubwa bandarini na hapa nimesikia na kujionea juu ya Uwekezaji kuanzia mitambo na Ufanisi wake mkubwa hapa ni niseme jambo moja wakati wa mjadala wa kupinga Uwekezaji Sisi tunaojua faida za Uwekezaji tuliwambia.

Leo kwa pamoja tunampongeza Mwenyekiti wetu na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM".

"Na CCM kwenye Nchi hii ndo tunawajibu wa kuwaletea maendeleo na kazi hii tumeifanya kwani wenzetu wao kazi Yao na wajibu wao ni kupinga na wamepinga vitu vingi SGR ,Ununuzi wa Ndege , Bwawa la Mwalimu Nyerere limepingwa lakini leo tunafaidi wote sasa niwaambie Wananchi wafahamu kuwa CCM ndio Chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo.

Lakini tangu Bandari yetu kupata Muwekezaji DP WORLD kuna mabadiliko makubwa ndani ya Miezi mitatu tu mfano muda wa kutoa makontena umepungua kutoka siku 46 za kusubili mpaka siku 0 yaani hakuna kusubili ikija inatia nanga moja kwa moja 

lakini utegemezi wa Bandari yetu kwa Nchi za Nje umekuwa mkubwa Nchi Nane( 8) na tayari Sudani Kusini ipo mbioni kuanza Kutumia Bandari yetu. Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla akizungumza baada ya kutembelea na kujionea kazi zinazofanyika Bandarini Dar es salam.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma kijavara amesema suala la Wafanyakazi limezingatiwa Wafanyakazi zaidi ya 350 wamehamia kwa Muwekezaji DP WORLD hivyo ni tofauti na maneno yalivyokuwa yanasemwa.