Makalla aipongeza Temeke kwa ujenzi wa Hospitali ya ghorofa Mbagala Rangi tatu

Na MWANDISHI WETU

KATIBU wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kwa kutekeleza dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Hospitali ya ghorofa sita ya Mbagala Rangi tatu,  iliyogharimu sh.bilioni 10, itakayo saidia utoaji huduma bora na kuondoa changamoto za afya kwa wananchi.

Pia, amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa Hospitali hiyo huku akiwataka kuongeza  kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Makalla ameyasema hayo, katika Jimbo la Mbagala alipokuwa akikagua ujenzi wa Hospitali ya Mbagara ya Rangi tatu, katika mwendelezo wa ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam.

"Naomba muongeze kasi ya utekelezaji ikamilike kwa wakati Mwezi Julia kama ilivyopanga, ikamilike watu wapate huduma njema za afya wananchi wapate huduma njema," alisisitiza.

Amesema kukamilisha mradi huo kwa wakati, kutasaidia Chama kuaminiwa na kupewa kura za kishindo katika Uchaguzi Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.

Ameeleza, mradi huo anaufahamu aliusimamia katika hatua za mwanzo akiwa Mkuu wa Mkoa na kuhakikisha anapatikana mkandarasi aliyekuwa na gharama nzuri.