Na MWANDISHI WETU
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave, amewataka wananchi wajitokeze kujiandikisha kupata fursa ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM.
Kilave ameyasema hayo, leo, wakati akiwasalimia wananchi wa Jimbo la Mbagala katika mkutano wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, katika Jimbo la Mbagala Wilaya ya Temeke.
Amesema hakuna chama kitakachoweza kufanya kazi zaidi ya CCM, hivyo wachague viongozi hao wa CCM, ambao watawaletea maendeleo, kama ambavyo Rais Dk.Samia anafanya.