MWENYEKITI UWT KIGAMBONI APONGEZWA UTOAJI WA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA CHAMA

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),  Kigamboni, Sikunjema Shabani, amesema mafunzo kwa viongozi wa yanaumuhimu mkubwa katika kukijenga Chama, huku akimpongeza Lilian Wasira  kwa kuandaa semini ya mafunzo hayo.

Ameyasema hayo wilayani humo, alipokuwa akigawa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo, kwa vingizi wa Chama wilayani humo,

Alisema Mwenyekiti Wassira ni kiongozi wa aina yake, ana upendo , jasiri, mbunifu na mchapakazi asiyechoka, kila siku yeye yupo kazini anapambana kuhakikisha chama kinajengwa.

Komredi Sikunjema ambaye alikuwa Mgenirasmi katika Mafunzo hayo alisisitiza wanawake kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanawake katika nafasi hizo  kuleta usawa. 

Alisisitiza, ushindi wa Rais Dk. Samia wanaoutaka 2025 ni wa kishindo na ishara itaanza kuonekana kupitia uchaguzi wa mwaka huu wa serikali za mitaa.