Mkurugenzi Igunga agawa mitungi ya gesi ya kupikia kwa wananchi

Na MWANDISHI WETU

IGUNGA - TABORA

Wananchi wilayani Igunga mkoani Tabora, wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia nishati safi.

Wito huo, ameutoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Abdalla Hamid baada ya kugawa mitungi ya gesi ya kupikia kwa baadhi ya wananchi wilayani hapa.

Akizungumza na wananchi hao, Selwa amesema lengo la kugawa mitungi hiyo ni kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia katika kampeni inayohamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo gesi na umeme na kuachana na nishati chafu hatua ambayo  itakiachia kizazi kilichopo na kijacho Tanzania iliyokua bora muda wote.

Selwa amegawa mitungi ya gesi katika kata ya Mbutu, Igunga, Nkinga, Mwashikumbili na Kining'inila.