CCM TANGA HAITAWAVUMILIA WATENDAJI WAZEMBE - RAJAB ABDALLAH

Na MWANDISHI WETU

CHAMA Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Tanga kimese hakita wavumilia watendaji wazembe wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ya kusimamia miradi ikamilika kwa wakati kuondoa changamoto zinazo wakabili wananchi.

Pia, amemwagiza Meneja wa Shirika la umeme (TANESCO), Wilaya ya Pangani kushirikiana na Ofisi ya Chama Wilaya hiyo kuhakikisha wananchi saba kati ya 29 wa  kitongoji Cha Madanga Ngambo, wanaunganishiwa umeme, baada ya kuwachangia fedha sh. 700,000.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Tanga, Rajab Abdallah ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama ,juzi alipokuwa anaendelea na ziara yake, mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

"Kuna mambo yalifanyika huko nyuma ambayo yamesababisha baadhi ya miradi kutokuwa vizuri, lakini kwa uongozi huu wa sasa wa Chama hatuwezi kuvumilia watendaji wazembe ambao hawaelewi kazi yao," amesema.