DORIS MOLLEL YALAANI TUKIO LA UKATILI DHIDI YA MTOTO WA MIEZI SITA DODOMA

Na MWANDISHI WETU

TAASISI ya Doris Mollel, imelaani tukio la kikatili la kubakwa hadi kufa lililotokea Dodoma, linalokiuka haki za msingi za mtoto na kuhatarisha mustakabali wa ustawi wa watoto nchini.

"Tunatoa pole kwa familia ya mtoto wa miezi sita aliyeuawa kikatili baada ya kubakwa na baba yake mzazi eneo la Mbuyuni, Kata ya Kizota, jijini Dodoma," amesema Doris Mollel.

Amesema matukio haya ya kikatili yamekuwa yakijirudia nchini hivi karibuni, hivyo, wanalaani vikali vitendo hivi vya kinyama na vya kukosa utu. 

Ameeleza kuwa, ukatili dhidi ya watoto, na hususani ukatili wa kingono, ni uhalifu wa kusikitisha unaovunja haki za kibinadamu na kuathiri vibaya maisha ya watoto.

Doris amesema, familia zao, na jamii kwa ujumla. Tunahitaji kuchukua hatua za haraka kuzuia matukio ya aina hii yasijirudie. Tunatoa wito kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi Tanzania, Kuharakisha uchunguzi na kuhakikisha kwamba baba huyu anachukuliwa hatua kali za kisheria kama mfano ili kuzuia matukio kama haya yasitokee tena.

Ameongeza, wataendelea kufuatilia matukio haya kwa ukaribu na kushirikiana na Jeshi la Polisi na Mahakama, kuhakikisha haki inatendeka. Tunasisitiza kwamba watoto wote wana haki ya kuishi kwa heshima, usalama, na utu. Tunaomba jamii nzima kushirikiana na serikali na vyombo vya usalama katika kupambana na ukatili wa aina hii.