Mwenyekiti CCM Tanga kuunguruma Tanga Mjini na Pangani

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, anatarajiwa kuunguruma katika Mkoa huo kwa siku tatu mkoani humo kupitia mkutano wa hadhara wa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Akizungumza leo, Mwenyekiti Rajab amesema wanatarajia kuanza mkutano huo, kesho Tanga Mjini  na kuendelea Septemba nne hadi tano, Pangani, mkoani humo.

Amesema wamejipanga vyema, maandalizi yako vizuri, kuhakikisha wanatekeleza dhamira ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha Chama na kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mwaka huu na ule wa mwaka kesho wa serikali za mitaa.