Na MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Afya, Jenister Mhagama, amesema hawataruhusu mtu yeyote kuchezea fedha zinazotolewa na serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kuwezesha huduma bora hivyo watakuwa wakali kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo kwa lengo kusudiwa.
Pia, amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Hospitali na Taasisi za Afya za Serikali ikiwemo Ile ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), huku akiahidi maboresho zaidi kutimiza azma lengo la kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi yaani utalii tiba.
Jenister ameyasema hayo, jijini Dar es Salaam, alipotembelea JKCI, kukagua uwekezaji uliopo na kuzungumza na wagonjwa wanaopatiwa huduma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Hospitali na Taasisi za Afya za Serikali.
"Kwakweli nisema, tutakuwa wakali, nitakuwa mkali katika usimamizi wa fedha zinazotolewa kwa matumizi ya mfumo wa bima ya afya kwa wote, hatuta mvumilia mtu yeyote anaye katisha mfumo wa fedha za bima ya afya kwa wote, kwani hiyo ndiyo ustawi wa Taifa," alisema.
Ameongoza mtu yeyote anayechezea na kukatisha mfumo wa bima ya afya kwa wote huyo hana nia njema na kwa wizara na Taifa, hivyo hawata mvumilia kwa namna yeyote katika suala hilo muhimu.
Ameeleza, watahakikisha wanasimamia vizuri mfumo matumizi ya fedha za bima ya afya kwa wote, zimetumike kwa mageuzi, matibabu na sehemu sahihi kufanikisha lengo kusudiwa bila kukatishwa na yeyote.