Ma MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Chacha Wambura, amewasititiza vijana na wananchi kwa ujumla kutunza amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa.
MNEC Wambura, ameyasema hayo Mkoani Geita, katika mkutano wa mafunzo ya fursa za uwekezaji katika madini, ikiwa ni mwendelezo wa Maonesho ya Teknolojia ya Madini mkoani humo.
Alieleza kuwa, katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuuu, wahakikishe tunadumisha amani na mshikamano kuepuka mtu au kikundi cha watu chenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aliwataka vijana, kuchangamkia fursa zilizopo za uongozi kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuuu, baada ya kujitathimini uwezo wao wakuwatumikia wananchi.