Na MWANDISHI WETU
Mbunge Balozi Liberata Mulamula, amesema Tanzania kushiriki katika jukwaa la kimataifa la G20, kupitia mwaliko kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kushiriki mkutano huo ni heshima ya kihistoria kwa nchi yetu katika muktadha wa kisiasa na kiuchumi.
Balozi Mulamula amesema umuhimu wake unaweza kuuangalia katika muktadha wa kutambulika kwa Rais Dk.Samia Kimataifa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza Diplomasia ya Uchumi.
"Kuimarika kwa ushirikiano wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa katika ngazi ya juu, kukomaa kwa siasa na Demokrasia nchini na ukuaji wa uchumi na maendeleo," amesema.
"Hii ni fursa adhimu ya Mhe. Rais wetu kukutana ana kwa ana au kwa ujumla wao na viongozi wa mataifa hayo makubwa na yenye uchumi mkubwa, duniani kubadilishana mawazo, pia, kuelezea dira yetu ya maendeleo na mikakati yetu ya kukuza uchumi na kuhamasisha uwekezaji na biashara kutoka kwenye hayo mataifa makubwa.