IGUNGA - TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwarahisihsia Watumishi majukumu yao yaliyokua yakifanyika kwa njia za kawaida na sasa yakitendeka kwa kutumia nyenzo anuai zikiwemo zile za Vishikwambi.
RC Chacha amaetoa Shukran hizo baada ya kugawa Vishikwambi kwa Maofisa Ugani baada ya kikao kazi na Maofisa hao, Watendaji wa Kata, Maofisa Tarafa , Madiwani wakiwemo viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amewataka kuhakikisha Vishikwambi walivyopewa na Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wanavitumia kujaza takwimu mbalimbali za serikali ikiwemo zile za zao la pamba na mazao mengineyo.
"Ndugu viongozi wenzangu, yote hayo ni mipango ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwarahisishia watumishi wa umma majukumu yao, hivyo tuendelee kumshukuru na kumpongeza Rais wetu kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya," ameomba.