KITE AWATAKA WANACHAMA KUJIANDAA NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na MWANDISHI WETU

Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Kite Mfilinge, amewataka viongozi na Wanaccm wa Wilaya ya Kibiti kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakao fanyika katika Vijiji na Vitongoji kuwapata viongozi wanaokubalika katika maeneo yao.

Kitte ameyasema hayo katika ziara ya Sekretarieti ya Mkoa iliyoanza leo,  kwa kukutana na viongozi wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuiya za Vijana, UWT na Wazazi na wazee maarufu katika Wilaya ya Kibiti.

Amesema kujiandaa mapema kwa uchaguzi ni ishara kubwa ya kukipatia Chama ushindi na kusisitiza kwamba ng'ombe hanenepi siku ya mnada.

Kitte amesema katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kila kiongozi anapaswa kujitathmini wapi alikosea na kuwakosea wengine kujifunza kusameheana.

Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani,  Mwanshamba Pashua amewasihi Viongozi hao kuendeleza Umoja na Mshikamano katika kuhakikisha Viongozi  watakaotokana na CCM wanashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024.