Na MWANDISHI WETU
OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Segerea, imewasilisha taarifa ya hali ya siasa katika jimbo hilo ikiwa ni hatua ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Taarifa hiyo iliwasilishwa na Katibu Ofisi ya Mbunge,Lutta Rucharaba ,kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya jimbo hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Akipokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya ya Ilala , Said Sidde,alisema taarifa hiyo ni muhimu kwani inatoa mwelekeo wa Chama katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi ujao.
Sidde, allimshukuru Mbunge Bonnah kuandaa taarifa kwa ustadi mkubwa hali itakayo saidia CCM kuibuka na ushindi katika jimbo hilo.
Akiwataka wajumbe kuzingatia yaliyowasilishwa na kutimiza matakwa ya Katiba ya CCM Ibara ya 5 kwa lengo la kushinda chaguzi na kuunda serikali .
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Sylivester Yared, aliwataka wajumbe kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao kwa kubuni mbinu zitakazo saidia Chama kushinda.
Kwa upande wa Mbunge Bonnah, aliwataka wajumbe kuimarisha umoja,ushirikiano na kuongeza kasi ya uwajibikaji.